MAGUFULI APANDA GHOROFA SABA ZA NEC KWA MIGUU KURUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ndugu John Pombe Magufuri amerudisha fomu ya kugombea urais wa Jamhuri katika ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) muda huu.
Katika tukio ambalo limekuwa na kivutio kikubwa kwa watumishi wa NEC, waandishi wa habari na wananchi waliokuwa wakipata huduma katika jengo la NEC ni kitendo cha mgombea huyo kuacha kutumia lift na kupanda ghorofa saba za jengo hilo kwa miguu.
Katika kile kilichoonekana kuwa ni kudhihirisha hali nzuri ya Afya yake, Magufuli amewataka viongozi wa CCM alioongozana nao katika tukio hilo wapande na kushuka kwa ngazi kama yeye.
Magufuli pia alikubali ombi la waandishi la kupiga nae picha ya pamoja ya Ukumbusho kabla hajatangazwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment