Saturday, October 19, 2013

*RAIS - AZINDUA KIWANDA CHA KUSINDIKA CHAI - LUPEMBE

 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua Kiwanda cha Chai kilichopo Ikanga, Njombe,  ikiwa ni sehemu ya  sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe. Rais Kikwete alianza ziara ya mkoa wa Njombe jana Ijumaa Oktoba 18, 2013.
 Rais Jakaya Kikwete akisikiliza maelezo kabla ya kuzindua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,  ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe  Ijumaa Oktoba 18, 201312: 
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai inavyotengenezwa katika kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,  baada ya kukizindua  ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe.
 Rais Jakaya Kikwete akikagua kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,  baada ya kukizindua  ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe.
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakikagua chai ikichambuliwa katika kiwanda cha chai  cha Ikanga, Njombe,  ikiwa ni sehemu ya  sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipata maelezo ya kiwanda kipya cha chai cha Ikanga, Njombe,  baada ya kukizindua  ikiwa ni sehemu ya sherehe za uzinduzi rasmi wa mkoa mpya wa Njombe.

No comments:

Post a Comment