Mshehereshaji wa Mjadala wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wenye kauli mbiu "The Future We Want" katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa mataifa kusheherekea miaka 68 ya kuanzishwa kwa Umoja huo akiwatambulisha Wachokonozi wa Mada Meza kuu Mh Janeth Mbene, Naibu waziri wa Fedha (wa pili kushoto) Bi. Dorothy Usili, Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA ( wa pili kulia), Paul Mashauri Mwenyekiti wa East Africa Speakers Bureau ( wa kwanza kulia) na Dakta. Lwidiko Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA).
.Ajira kwa vijana si bomu kama watapata mafunzo ya ujasirimali na mitaji
.Serikali yaahidi kuendelea kusaidia vijana kwa maslahi mapana ya taifa
Na Moblog Team
SERIKALI imewataka vijana kuachana na fikra potovu za kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake wafikiri zaidi kujiajiri ili kuweza kupambana na kuondoa kabisa tatizo la ajira nchi. Moblog inaripoti.
Kwa muda mrefu watu wa kada mbalimbali wasomi, viongozi wa dini na wanasiasa wameonya kwamba tatizo la ajira kwa vijana nchini ni bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote kutokana na ukweli kwamba fursa za ajira zimekuwa chache nchini.
Akizungumza kwenye Mjadala wa Wazi katika kusheherekea Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa mataifa jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janet Mbene amesema asilimia 75 ya watu hapa nchini ni vijana chini ya umri wa miaka 35 ambayo ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Pichani juu na chini ni Naibu Waziri wa Fedha Bi. Janeth Mbene akitoa mada yake juu ya mstakabali wa Vijana katika kupambana na tatizo la Ajira nchini na nafasi ya Serikali katika kuwasaidia vijana kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
0 comments:
Post a Comment