BIN ZUBEIRY BLOG
Friday, January 31, 2014
KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana Joseph Mwaisango.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment