Bw.Herve’ Joly ambaye ni Mkurugenzi msaidizi na Mkuu wa idara ya Afrika sehemu ya Mashariki akishauriana na mwenzake baada ya kupokea hoja kutoka kwa Dr. Servacius
Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali.
KILA mwaka Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la
Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii
imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake hapo tarehe 13, mwezi Octoba,
2014.Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na
kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile ndiye
kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye anawakilisha kama Gavana mbadala
(Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii.
Mikutano hii inatoa nafasi ya
kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa
kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na
matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya kuboresha
uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza kutusaidia kuboresha
na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi. Maeneo ambayo
yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji fedha, mapato ya
nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha.
Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na
mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira.
Hali
ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi na
manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji
-Wizara ya Fedha
Washington
D.C
7/10/2014
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu yuliohusu masuala na fedha na sera ya kiwango cha ubalilishaji fedha.
No comments:
Post a Comment