MAMBO YA MSINGI KATIKA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU

Na Dominick salamba, DAR ES SALAAM
KUMEKUWA na tambo, vijembe na dhihaka mbalimbali baina ya mashabiki wa soka huku kila mmoja akijinasibu kuwa timu yake ndio imeweka kambi ya maandalizi ya msimu katika eneo bora na kudhihaki kambi ya upande mwingine. 
Si jambo baya maana ndiyo miongoni mwa mambo yanayoleta msisimko na kuchochea hali ya ushindani baina ya timu moja na nyingine. Hivyo nimeona nikupe kidogo mambo ya muhimu ili hata ikitokea timu yako kutofanya vizuri  uwe na uwanja mpana wa kipima na kujua kama kipindi cha maandalizi mambo ya msingi yalizingatiwa, na je kambi ilikuwa sehemu sahihi?ilipendekezwa na benchi la ufundi?vifaa muhimu vya kujifunzia vilipatikana?utulivu ulikuwepo?na mengine mengi badala ya kuanza kuangalia kambi mmenda na bajaji,bodaboda,gari au ndege.

Kuna wakati tumeshudia timu zikianzia ufukweni,na maeneo mengine hasa waalimu wakiangalia zaidi maeneo ambayo wanatamani kuyaboresha kuzingatia ripoti ya msimu uliyopita lakini pia kuzingatia aina ya wachezaji walipo,na wale ambao wamesajiliwa uku idadi ya waliongezwa na waliopo kikiwa ni miongoni mwa vigezo muhimu katika kuangalia aina ya maandalizi ya msimu ujao.
Haiishii hapo tu pia tunakwenda mbali na kuangalia hali ya hewa itakayotumika wakati wa mashindano ili kuchagua eneo ambalo litakuwa na mfanano na maeneo ambayo mashindano yatafanyika na kutengeneza utimamu wa miili kulingana na mazingira husika.
Siyo hapo tu pia kuangalia ukubwa wa mashindano kwa maana ya idadi ya mechi na kipindi cha maandalizi ili kupata mwendelezo wa viwango vya wachezaji sambamba na kuviboresha sambamba na ukubwa wa mashindano kwa maana ya idadi ya mechi na vipindi vya majira ya eneo husika mfano Tanzania tunapitia vipindi viwili mpaka vitatu ili kuukamilisha msimu wa ligi kwa kuanzia msimu wa joto,baridi na kipindi cha mvua hivi vyote wachezaji hao hao watatakiwa kukabiliana navyo na kupata matokeo pia
Hivyo kuelekea mwanzo wa msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.ambao utaanza tarehe 17/08/2019 ikiwa ni mechi ya ngao ya jamii na baada ya hapo tarehe 23/08/2019 ligi itafunguliwa rasmi. 
Timu mbalimbali zimeanza maandalizi ya msimu ujao na hapa tunakuletea mambo ya kuzingatia katika maandalizi na umuhimu wake.
1. Muda wa mafunzo katika kambi ( duration of training camp).
2. Kupata mechi za kujipima nguvu.
3. Kujikita katika kujenga utimamu wa wachezaji ( Focused fitness session).
4. Kuwa na mafunzo yatakayo imarisha afya za wachezaji katika matumizi ya nguvu kulingana na wakati husika (all around training focus on energy system).
5. kujenga wepesi wa wachezaji na kuwa na pumzi ya kutosha wakati wote wa mchezo ( training to increase ventitatory threshold).

UMUHIMU WA MAANDALIZI YA MWANZO WA MSIMU (Pre-season)
1. kuongeza ujuzi (maarifa kwa wachezaji).
2. kuzuia uwezekano wa majeraha ya mara kwa mara baada ya msimu kuanza.
3. kuimarisha utimamu wa mwili.
4. kutengeneza muunganiko wa timu.
5. kujenga hali ya ushindani ndani ya timu na hamasa ya kupata matokeo.
6. kupata kikosi cha kwanza na kujua mbadala wa wachezaji wa kikosi cha kwanza.
7. kutengeneza mahusiano ndani ya timu.

Hivyo basi achilia mbali mambo mengine ya nje ya uwanja mahali kambi imewekwa na mengine mengi jambo la msingi ni kuhakikisha malengo juu ya timu yanafikiwa kama ambavyo benchi la ufundi limependekeza.

(Dominick Salamba ni mchambuzi wa michezo, pia anapatikana katika Instagram akaunti kupitia @dominicksalamba au nambari +255 713 942 770)
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments: