CHONGOLO AFANYA ZIARA MLELE MKOANI KATAVI


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Daniel Godfrey Chongolo akisalimiana na Chifu wa Kabila la Wakonongo, mwenye utawala wa eneo la Kalovya, Chifu Michael Kayamba, leo Jumatano Oktoba 5, 2023, baada ya Ndugu Chongolo kuwasili Jimbo la Katavi, wilayani Mlele, kutembelea na kukagua mradi mkubwa wa Bwawa la Nsenkwa, linalojengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji safi na salama kwa matumizi ya wananchi wa vijiji 16 katika Halmashauri ya Mlele mkoa wa Katavi. Mradi huo utakaowahudumia takriban wakazi 68,000 utagharimu jumla ya Sh. 2.8 bilioni.

Akiwa katika eneo hilo la mradi, Katibu Mkuu Komredi Chongolo, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa bwawa hilo kutoka kwa Watendaji wa Wizara ya Maji, Ruwasa, Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mlele, waliobuni mradi huo, aliwapongeza kwa kubuni jambo litakalokuwa na matokeo makubwa na chanya kwa wananchi, kwa gharama ndogo.

Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment