Wednesday, October 18, 2023

TET NA TAKUKURU WAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imeingia makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kuwezesha utoaji wa elimu ya kuzuia na kupinga rushwa kwa wakuza mitaala, walimu, wanafunzi na waandika vitabu.

Katika Makubaliano hayo, TAKUKURU na TET watatoa mafunzo kwa waandishi wa vitabu vya shuleni na waandishi wengine wa maudhui yanayopinga rushwa juu ya namna ya kuingiza masuala ya kupinga rushwa katika maandiko mbalimbali.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TET ,Dkt. Aneth Komba amesema kupitia makubaliano hayo wataunda timu ya kutathmini utekelezaji wa mtaala unaozingatia masuala ya kupinga Rushwa.

Amesema kupitia ushirikiano huo wataweza kuwafikia wanafunzi na walimu ambao wanatarajia watasaidia kuiambukiza jamii kwa ujumla kuwa na tabia njema, maadili mema na tabia ya kuzuia, kupinga na kuikataa rushwa.

"Ninaamini kuwa kupitia ushirikiano huu jamii itapata uelewa na mambo mbalimbali yahusianayo na rushwa ikiwemo maana ya rushwa, aina za rushwa, athari za rushwa na njia za kupinga na kupambana na rushwa. hakika jambo hili litachangia kujenga kizazi chenye maadili na kinachokataa na kupinga rushwa". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni amesema kuwa wakitumia njia isiyo rasmi ya kutoa elimu shuleni kwa kutumia klabu mbalimbali ambapo katika mwaka huu jumla klabu 1,0736 zilianzishwa zenye washiriiki milioni 1.09, hivyo kupitia ushirikiano huo wataongeza jitihada kudhibiti suala hilo.

Hata hivyo amesema kuwa vijana wakishirikishwa wanaweza kupinga rushwa kwa wapandikiziwe utlii na uzalendop waone kuwa suala hilo halilusiwi.

"Ushirikiano na makubaliano haya tutayatendea kazi sio katika makaratasi tu bali kwa vitendo hivyo kuwezesha wanafunzi kuwa na uelewa juu ya rushwa na kuwezesha kuwafichua wla rushwa". Amesema
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni wakisaini Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba (kushoto) akibadilishana mikataba na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni mara baada ya kusaini Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni wakionesha mikataba waliosaini ya Makubaliano ya Ushirikiano wa pamoja leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakifuatiliana hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya TAKUKURU na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wakifuatilia hafla ya Utiaji saini Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba akizungumza wakati wa hafla ya Utiaji saini Makubaliano ya Ushirikiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TAKUKURU na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ,Dkt. Aneth Komba na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP. Salum Hamduni wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano kati ya TAKUKURU na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) leo Oktoba 18,2023 Jijini Dar es Salaam.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:

Post a Comment