Saturday, November 4, 2023

DKT. ABBASI AWAPOKEA WAWEKEZAJI WAKUBWA WA WAKIMAREKANI, ATOA NENO


Na John Mapepele

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii na Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya The Royal Tour, Dkt. Hassan Abbasi amepokea ujumbe wa awali wawekezaji wakubwa na watu maarufu zaidi ya 180 kutoka nchini Marekani.

Dkt. Abbasi amepokea ujumbe huo leo akiwa makamishna wa TANAPA na Hifadhi ya Ngorongoro kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) asubuhi ya leo walipotua kwa Shirika la ndege ya la Oman huku akisisitiza watendaji wote wa Taasisi zilizochini ya Wizara kutoka ofisini na kuwakarimu wageni.

"Kama kuna kitu ambacho kwa sasa tunakitaka ni watendaji kutoka kuwahudumia wageni wetu, kwa kuwa kama Mhe. Rais ameweza kutoka na kuandaa Royal Tour sisi ni nani tusitoke". Ameongeza Dkt. Abbasi

Wawekezaji hao wanatarajia kutembelea vivutio mbalimbali nchini ikiwemo Hifadhi bora Afrika kwa mara tano mfulululizo Serengeti pamoja na kivutio bora Afrika kwa mwaka 2023 na Hifadhi ya Ngorongoro.

Aidha, amesema sekta ya Utalii nchini imevunja record mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ongezeko ambalo halijawai kutokea. Takwimu zinaonesha kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 tulipata jumla ya watalii 1,638,850 walioingizia taifa mapato ya jumla ya shilingi bilioni 522.7 ikilinganishwa na watalii 1,123,130 walioingizia taifa mapato ya shilingi bilioni 290.4 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 45.9 ya watalii na mapato asilimia 80.

Ameongeza kuwa pia lipo ongezeko kubwa la watalii na mapato kwa kipindi cha Januari hadi Juni, 2022/2023 ukilinganisha na kipindi kama hicho 2020/2021. Kutoka 575,397 na mapato ya shilingi bilioni 130,592,796,544 Januari hadi June, 2022 hadi kufikia watalii 759,327 na mapato shilingi bilioni 202,375,961,009 Januari hadi Juni, 2023.

Akizungumza mtendaji mkuu wa Kampuni ya Goshen Safari iliyowaleta wageni hao Peter Robert amesema ukuaji wa utalii unatokana na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na mikakati mbalimbali iliyowekwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na wadau mbalimbali.

Katika hatua nyingine amesema Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa ziara ya wacheza tennis maarufu iitwayo McEnroe Luxury Safari Tour itakayohusisha mashindano ya mchezo wa tennis yatakayofanyika katika Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Ziara hii itawezesha kujumuika na wachezaji maarufu wa mchezo huo Bw. John na Patrick McEnroe.

Amesema tukio hili la mchezo wa Tennis katika Hifadhi ya Taifa Serengeti linalenga kuongeza thamani kwa aina hii ya utalii ambao ni moja za mazao yanayopewa kipaumbele na Wizara ya Maliasili na Utalii. Utalii wa michezo ikiwemo Tennis umeendelea kuwa maarufu kwa watu binafsi kutembelea maeneo mapya, kupata uzoefu wa tamaduni tofauti na kushiriki katika shughuli zinazohusiana na utalii wa michezo.

No comments:

Post a Comment