Dkt. Yonazi aridhishwa na maandalizi ya Kuelekea Siku ya UKIMWI Duniani

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea maandalizi yaliofanywa na wadau mbalimbali kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika 1 Disemba,2023 katika Viwanja vya Morogoro Sekondari ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(mb).

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI"

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo na kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI Nchini.
Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment