TAMASHA la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) linatarajiwa kufanyika kwa siku nne ambapo litafunguliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro Oktoba 23, 2024 katika Viwanja vya TaSUBa.
Tamasha hilo litahusisha shughuli mbalimbali za kisanii, kiuchumi na kijamii. Lengo kuu likiwa kuvutia wadau na watazamaji kutoka ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 22, 2024 Bagamoyo, mkoani Pwani Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, amesema tamasha hilo limekuwa na mafanikio makubwa kuhakikisha wanaendeleza sanaa.
Amesema anatarajia wasanii wote watakaoshiriki watatoa burudani ya aina yake na kukata kiu ya mashabiki wao.
“Tamasha limeshakuwa na mafanikio makubwa kwa wasanii na sanaa yetu kwa ujumla, tunatarajia mwaka huu kutakuwa na burudani tofauti kutoka mataifa mbalimbali ambao pia wamekuwa wakishiriki,” amesema
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya TaSUBa, Dkt. Herbert Makoye amesema tamasha la msimu huu linatarajiwa kuhusisha vikundi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi vikiwemo vya ngoma za asili, muziki wa asili na wa kisasa, maigizo, sarakasi, ushairi, vichekesho na mazingaombwe.
Amesema kuwa pia katika tamasha la hilo mwaka huu kutakuwa na wafanyabiashara watakaokuwa na bidhaa mbalimbali za asili.
“Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani maandalizi yote yalishakamilika na kwamba tunatarajia litahusisha wasanii kutoka ndani nan je ya nchi.
“Pia wageni wote watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio na utalii yakiwemo Mji Mkongwe, Kaole Ruins, Caravan Serai na Boma la Wajerumani,” amesema.
Ameongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na mada mbalimbali zitakazojadiliwa zikilenga kuwainua wasanii na kuwajengea uwezo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga amesema kuwa wamejipanga vyema kuhakikisha wanaimarisha usalama zaidi na kila atakeyeshiriki tamasha hilo ataondoka salama.
“Niwatoe wasiwasi wadau wa sanaa na utamaduni kwamba tumejipanga vyema kuhakikisha usalama unaimarishwa na kila atakayehudhuria ataondoka salama,” amesema.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 22, 2024 Bagamoyo mkoani Pwani wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Tamasha la 43 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambalo litafanyika Oktoba 23-26, 2024 katika viwanja vya TaSUBa.

No comments:
Post a Comment