IMEWEKWA JULAI 31, 2013 SAA 3:11 USIKU
NYOTA Gareth Bale amempasukia usoni Andre Villas-Boas na kumwambia kwamba anataka kuondoka Tottenham na kujiunga Real Madrid wakati huu wa kiangazi.
Taarifa hii ni mbaya kwa Tottenham hasa ikiwa hii ni siku ya kwanza ya staa huyo wa Wales kwenye mazoezi ya klabu hiyo, baada ya ofa ya pauni milioni 85 kuwekwa mezani na miamba hiyo ya Hispania.
Mkurugenzi wa Michezo wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kwamba Bale anastahili kuachwa kutimiza ndoto yake ya kujiunga na Real Madrid, na kuongeza kwamba anaweza kuwa mchezaji bora wa dunia kama akitua Bernabeu.
Anaondoka: Gareth Bale amemwambia kocha wa Spurs, Andre Villas-Boas kwamba anataka kuondoka
Ndani: Bale akiwasili kwenye uwanja wa mazoezi wa Spurs jana asubuhi
Anatoka: Bale akiondoka nyumbani kwake Essex, Jumatano asubuhi na kwenda mazoezi Tottenham
Straika wa Wales anataka kuondoka, lakini hataki kuweka mezani maombi rasmi ya kuondoka Tottenham.
Msimu uliopita alipata tuzo zote mbili ya Mchezaji Bora wa Kulipwa na ile ya waandishi wa habari na tayari anatajwa kama mmoja kati ya wachezaji bora duniani.
Spurs wameshangazwa na mabadiliko ya ghafla ya Bale, 24, tangu Real walipolivalia njuga suala lake.
Ni wiki iliyopita tu walikuwa wakiamini kwamba atasaini mkataba mpya na uhusiano wake mzuri na Andre Villas-Boas utamshawihi kubaki.
Lakini hiyo ilikuwa kabla ya Real hawajamfungulia Zidane, ambaye alisema kwamba siyo ajabu kwa mchezaji kuchachawa akisikia kwamba anatakwa na Real Madrid kwa sababu ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi nyeupe za Real Madrid.
Huku akiongeza kuwataka Spurs wamuache Bale akae meza moja na Real wazungumze kwa sababu nafasi kama hiyo huja mara moja tu maishani, na kumalizia kusema kwamba Bale yuko levo za kina Ronaldo na Messi na anastahili kucheza ligi ya mabingwa Ulaya na kushinda mataji, na kuwa mchezaji bora wa dunia.
Hacheki mtu: Bale, ananafasi ya kuwa mchezaji ghali duniani, anawaza mengi hapa
Hakuna shaka kwamba Madrid wako radhi kutoa kiasi cha pauni milioni 85 kwa ajili ya Bale, lakini Mwenyekiti Daniel Levy anataka kuona ofa pauni milioni 100.
Licha ya tabia ya Bale kubadilika hawezi kufanya yale yaliyefanywa na Luka Modric kiangazi mwaka jana kwa kuondoka kwenye timu kulazimisha uhamisho wake Real.
Na sasa hivi Madrid wanatamani Bale kufanya tabia kama zile za Modric.
Uwepo wa Modric kwenye kikosi cha Madrid utamsaidia Bale kuzoea haraka mazingira mapya ya Bernabeu kama akihamia huko.
Lakini kocha wa zamani wa England na Spurs, Glenn Hoddle anahisi kwamba Bale hayupo tayari kwenda kucheza nje ya England.
Hoddle anaamini kila mchezaji anathamani yake, lakini anaamini itakuwa vizuri kwa Bale kuendelea kubaki Tottenham kwa sasa na kuendelea pale alipoishia kwenye msimu wa 2012-13.
Huyooo: Bale amezungumza na Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy baada ya kubadili mawazo na kutaka kwenda Hispania
Mazungumzo: Bale (Juu) atazungumza kuhusu mustakabali wake na wakala Jonathan Barnett (picha ya chini kushoto) na Daniel Levy (kulia) na kuna kila dalili kwamba Levy atalazimika kukubali maombi ya Bale kama ofa ya maana zaidi itakuja.
Njoo: Zinedine Zidane (Kulia), akiwa na kocha wa Real, Carlo Ancelotti, wanaongoza mashambulizi ya kunasa Bale
Hoddle, ambaye anajua inafananaje kuondoka Spurs na kutoka nje ya England, baada ya kuihama Spurs na kwenda Monaco mwaka 1987, aliongeza kusema kwamba ni kitu rahisi kuonyesha kiwango cha juu, lakini kubaki na kiwango hicho ndiyo kazi zaidi.
Hoddle alisema “Hofu yangu ni kuwa amekuwa akipata tisa ya 10 katika kila mechi, baadhi ya mabao amefunga yamekuwa ya kuvutia sana, na ndio maana watu wako tayari kulipa fedha nyingi kwa ajili yake na mashabiki wa Real Madrid watakuwa wanaamini kuwa naye na Ronaldo kwenye kikosi kimoja kunaipa timu nafasi ya kutoa upinzani Ulaya tena.
“Unapoenda nje ya nchi miezi minne, mitano, sita ya mwanzo inakuwa migumu sana kufikia kiwango kile na kama familia yake itakuwa mbali atapata wakati mgumu zaid. Nahisi anaweza kuwa na msimu mbaya, kama anataka kwenda kucheza soka ni bora asubiri mwaka mmoja au miwili.”
Mstari wa kuingia uwanjani: Kocha Tottenham, Andre Villas-Boas anahaha kumbakiza mchezaji wake muhimu
Rekodi ya dunia: Dili ya kumnasa Bale itafunika dau la pauni milioni 80 ambalo Real walilipa kwa ajili ya Cristiano Ronaldo mwaka 2009
Nainua mikono: Bale anawazo moja tu kwa sasa kwenda Real Madrid na siyo Manchester United
Njiani: vyombo vya habari vya Hispania vinaanza kutabiri ujio wake
Tangazo: Bale bidhaa adimu sokoni kwa Spurs, bango lake liko Times Square, New York
0 comments:
Post a Comment