Na Ali Issa,Maelezo Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Ali Mohamed Shein leo alikuwa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar walio hudhuria Mazishi ya walio kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ Sajenti Shaibu Shekhe Othuman na Koplo Mohamed Juma Ali Wenye asili ya Zanzibar walio fariki dunia kwa shabulizi la kushutukiza na waasi wakati wakilinda Amani Nchini Darfur.
Dkt Shein akiambatana Wananchi na viongozi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwemo Makamo wa Pili Rais Balozi Seif Ali Iddi ,Wazi wa Ulizi Tanzania Shamsi Vuai Nahodha ,Waziri wanchi Afisi ya Rais Ikulu mwinyihaji Makame Mwadini, Mkuu wa Mkoa Mjini magharibi Abdalla Mwinyi Khamis Bregedia Jeneral Kamanda wa Bregedi ya Nyuki Sharif Sheikhe Othuman na wakuu wa Vikosi vyote vya Ulizi na Usalama hapa Zanzibar.
Mazishi hayo yakiambatana na sala ya Maiti iliosaliwa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Noor Muhamad S.A.W ulioko Mombasa Mjini Unguja, yalielekea Mwanakwerekwe kwa Mzishi yakiongozwa kwa Gwaride la Jeshi kwa mwendo wa pole na kutoa salamu zao za Mwisho.
Wakitoa salamu za Rambi rambi ASP Luten Sabato Devid okoku na FA Kepten Franki Adam Mtwazi kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kua, amestushwa na kuhuzunishwa kwa tukio la Jumamosi Julai 13 wiki iliopita ambalo lilifanywa na waasi na hatimae kupoteza maisha kwa askari wao Saba kitu ambacho si kimetia huzuni kwa familia bali hata kwa Taita la Tanzania, hivyo wako pamoja kwa kuomboleza katika kipindi hiki kigumu.
Wamesema Sajent Shaibu na Koplo Mohamed watakumbukwa daima kutokana na mchango wao walio utoa katika uhai wao wakiwa watumishi wa taifa hili na Mataifa Mengine ya Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.
Wakitoa wasfu wa MP 72 Shaibu Sheikhe alizaliwa mwaka 1972 katika kijiji kiitwacho Urusi kiliopo mkoa wa Mjini Magharibi na alipata Elimu yake ya Msingingi kijijini hapo na kumaslizia elimu yake ya sekondri katika skuli ya Bembela mwa 1991na alijiunga na jeshi hilo mwaka 1992 .Sajenti Shaibu ameowa na ameacha mke na watoto wanne .
Koplo Mohamed alizaiwa 1981 huko pemba katika kijiji kiitwacho Konde na alipata Elimu yake ya msingi na sekondari katika skuli ya Miti ulaya mwaka 1989 -2002 na alijiunga na jeshi la wana nchi Tanzania akiwa ametumikia kwamuda wa miaka 11na siku kuminambili hadi kufa kwake, ameacha mke na mtoto mmoja.Muungu aziweke Roho za Marehemu Peponi Amini.
Katika hali isiyotarajiwa miongoni mwa gari zilizokuwa zikienda mazishini gari moja aina ya Rova namba JW 2955 kutoka kikosi cha 101 ilipata ajali katika maeneo ya Mwanakwerekwe na kujeruhi watu 19 wakiwemo askari watatu wa JWTZ.
Ajali hiyo ilisababishwa na msongamano wa magari ambapo iliacha barabara na kuanguka baada ya dereva aliyejulikana kwa Salim Mansur MT 98501 kushindwa kuidhibiti gari hiyo.
Baada ya Ajali hiyo majeruhi hao walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
iliyokuwa imebeba wanajeshi na Raia kwa ajili ya mazishi na kujeruhi imeelezwa kuwa wakati marehemu hao wakipelekwa mazishini Gari ya Askari hao aina Rova ikiwa imebeba askari na wana nchi waendao mazikoni ilianguka mwana kwerekwe ikidaiwa gari hiyo kupakia watu wengi iliopelekea kuzidi mzigo na kupinda krosi karibu na eneo la mazishi Gari hiyo ilianguka na watu kuumia vibaya badhi yao
Masjid Nuur Muhammad (SAW) ndio Mskiti walioswaliwa wanajeshi wa aliouwawawa huko Darfur katika harakati za kulinda amani chini ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (Unamid),ulioko kwa mchina nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi mbalimbali wakiswalia maiti za wanajeshi wawili wa Zanzibar waliofari Darfur Nchini Sudan. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Dereva wa gari la JWTZ lililopata ajali katika eneo la Mwanakwerekwe wakati wa wakielekea kwenye mazishi ya wanajeshi wawili wa Zanzibar waliofari Darfur akishushwa kwenye gari katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajili ya kupatiwa matibabu. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).
Picha no. 06 Wanajeshi wakimshusha majeruhi wa ajali ya gari ya JWTZ iliotokea Mwanakwerekwe , katika hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanzibar).

0 comments:
Post a Comment