Kamanda wa Kikosi cha Polisi wa Bandari ya Zanzibar, akiongoza Operesheni ya kukagua magunia yaliyokuwa na Pembe za Ndovu yaliyokamatwa katika Bandari hiyo jana asubuhi yakiwa katika harakati ya kusafirishwa nje ya Nchi kupitia bandari hiyo, zoezi hilo limefanywa chini ya Jeshi la Polisi Bandari Kikosi cha KMKM, yakiwa katika Kontena la futi 40.
Askari wa jeshi la Polisi wakitoa Pembe za Ndovu katika magunia wakati wa zoezi hilo jana asubuhi katika bandari ya Malindi Zanzibar.
Magunia yaliyosheheni Pembe za Ndovu na makombe ya pwani yaliyokuwa yamehifadhiwa katika Kontena likiwa tayari kusafirishwa nje ya Nchi, na kukamatwa katika bandari ya Zanzibar, jana.
Zoezi likiendelea kupekuwa magunia ya Makombe ya Pwani kutowa magunia yaliyohifadhiwa Pembe hizo.
Baadhi ya Pembe za Ndovu zilizokamatwa katika Bandari ya Malindi Zanzibar.
Askari wakiendelea kuhesabu pembe hizo za Ndovu zilizokamatwa katika Bandari ya Zanzibar ili kupata thamani yake halisi.
Kila gunia likipimwa kupata uzito wake wote. IMEHAMISHWA KUTOKA ZANZINEWS
0 comments:
Post a Comment