CCM YATAJA KAMATI YA USHINDI UCHAGUZI MKUU, MWENYEKITI KINANA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo kimetangaza kamati yake ya kampeni itakayofanya kazi ya kukitafutia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Kamati hiyo yenye majina 32 itaongozwa na Abdulrahiman Kinana, Rajab Luhwavi, Makamu Mwenyekiti Bara na Vuai Ali Vuai, Makamu Mwenyekiti Zanzibar. Anaandika Pendo Omary …(endelea).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kwa vyombo vya habari inasema “uteuzi wa majina 32 ya kamati hiyo ulitokana na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika jana katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.”
Pia, kikao hicho kilikamilisha uteuzi wa wagombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho katika majimbo ya Singida Mashariki ambapo ameteuliwa Jonathan Njau na Kiteto ambapo ameteuliwa Emmanuel Paplam.
Katibu Mwenezi wa CCM, Ndugu Nape Nnauye

KAMATI YA KAMPENI YA CCM
Abdulrahiman Kinana – Mwenyekiti
Rajab Luhwavi – Makamu Mwenyekiti Bara
Vuai Ali Vuai – Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Sofia Simba
Mohamed Seif Khatib
Asha – Rose Migiro
Samuel Sitta
Nape Nnauye
Mwigulu Nchemba
Harrison Mwakyembe
January Makamba
Amina Makillagi
Chrstopher Ole Sendeka
Stephen Wasira
Abdallah Bulembo
Hadija Aboud
Mohamed Aboud
Lazaro Nyarandu
Issa Haji Ussi
Waride Bakari Jabu
Mahmoud Thabit Kombo
Shamsi Vuai Nahodha
Maua Daftari
Stephen Masele
Pindi Chana
Shaka Shaka
Makongoro Nyerere
Bernard Membe
Sadifa Juma Khamis
Antony Diallo
Livingstone Lusinde
Ummy Mwalimu
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment