Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Eliezer Feleshi akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msoffe.
Washiriki wa kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023. Kongamano hilo limeandaliwa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msoffe akizungumza wakati wa kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Griffin Venance Mwakapeje akitoa hotuba fupi wakati wa kufunga kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Eliezer Feleshi (wa tatu kushoto) akifurahia jambo na viongozi wengine wakati wa kufunga kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Eliezer Feleshi (wa nne kushoto) akiwa na viongozi wengine wakati wa kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt Eliezer Feleshi akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma tarehe 4 April 2023. Katikati ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Griffin Venance Mwakapeje.
****************
Na Mwandishi Maalum
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi ametaka kuwepo ushirikiano baina ya serikali na wadau zikiwemo taasisi za dini katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili nchini.
Aidha, alieleza kuwa, viongozi wa dini nao wanao wajibu na mchango mkubwa wa kukemea mmomonyoko wa maadili pamoja na makosa ya kimaadili huku akisisitiza taasisi za dini kuwa na wajibu wa kutoa taarifa wanapoona vitendo vya unyanyasaji au ubakaji vikitoa.
‘’Wajibu na mchango wa kukemea mmomonyoko wa maadili unazifanya taasisi za dini ni kwa nini zitambuliwe na serikali na kwa ujumla serikali na taasisi hizo vinategemeana’’ alisema Dkt Feleshi.
Dkt Feleshi alisema hayo tarehe 4 April 2023 wakati akifunga kongamano la siku moja la tathmini ya utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili lilofanyika jijini Dodoma.
Pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelitaka jeshi la polisi nchini kuimarisha upelelezi katika matukio yanayoripotiwa ili kuondoa mianya ya washitakiwa wasiostahili kushitakiwa mahakamani.
‘’Kupitia kongamano hili naiomba jamii ishirikiane na jeshi la polisi katika kuhakikisha matukio yanayoripotiwa yanafikishwa mahakamani kwa haki’. alisema Dkt Feleshi.
Aliipongeza Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kwa kuandaa kongamano alilolieleza kuwa litaisaidia kutimiza malengo yake ya kufanya maboresho ya sheria mbalimbali hasa ikizingatiwa kuwa, kwa sasa kumekuwa na ukiukwaji wa maadili ikiwemo makosa makubwa ya ubakaji, ulawiti pamoja na udhalilishaji wa wanawake na watoto.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Griffin Venance Mwakapeje amesema, Tume yake imeanza kufanya makongamano kwa kushirikiana na wadau kwa lengo la kufanya maboresho ya sheria na kuijenga Tanzania kwa pamoja.
Aliwapongeza washiriki wa kongamano hilo kwa kutoa michango aliyoieleza kuwa itasaidia katika kuboresha Sheria za Makosa dhidi ya Maadili.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Mstaafu January Msoffe alisema, kongamano hilo la siku moja limeipa uzoefu Tume na kusisitiza kuendelea na makongamano ya aina ili kufanya maboresho ya sheria yanayotokana na maoni ya wadau.
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeandaa kongamano la siku moja la Tathmini ya Utekelezaji wa Sheria za Makosa dhidi ya Maadili ili kukutana na wadau wakiwemo watekelezaji wa sheria kwa lengo la kupata maoni yatakayowezesha kutoa mapendekezo.
Katika masuala ya utafiti na tathmini, Tume imeandaa maandiko ya tahmini ya utekelezaji wa sheria mbalimbali ili kubaini endapo malengo yaliyokusudiwa kwa kutungwa sheria hizo yamefikiwa.
0 comments:
Post a Comment