RC MAKALLA AONGOZA MKUTANO WA WADAU WA MAZINGIRA


Viongozi wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka wakiwa katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mwanahamisi Mnkunda akizungumza katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya akiwa katika Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbaali wa Mazingira wakiwa kwenye mkutano kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira leo Aprili 14,2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)

******************

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ameongoza Mkutano na Wadau wa Mazingira kujadilia suala la viwango vya udhibiti wa kelele na mitetemo pamoja na katazo la mifuko ya plastiki leo tarehe 14 April 2023, uliohudhuriwa na wadau mbalimbali wa mazingira katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Mkutano huo, Mhe.Makalla amesema kuna umuhimu mkubwa viongozi wa dini wakapatiwa elimu kusimamia katazo na zuio la mifuko ya plastiki pamoja na udhibiti wa makelele kwenye maeneo ya makazi ya watu ili kuondoa changamoto hizo ambazo zimekuwa zikitokea katika maeneo mbalimbali kwenye Jiji la Dar es Salaam.

Mhe. Makala amesisitiza juu ya changamoto ya viwango vya juu vya kelele katika kumbi za starehe na nyumba za ibada pamoja na kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki akiwaasa wanajamii kuepuka matumizi ya mifuko hiyo kwani ni chanzo cha uharibifu wa mazingira na kutoa muda wa wiki moja kwa NEMC na TBS kuweka ratiba ya kupita katika wilaya za jiji la Dar es salaam kufanya ukaguzi wa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mifuko ya plastiki.

Amesema "Dar es salaam bila mifuko ya plastiki na kelele zilizodhidi viwango inawezekana na ni wakati wa kila mmoja kuwajibika na kuhakikisha haki inatendeka bila kupepesa macho na kwa wazalishaji kusalimisha mifuko ya plastiki waliyoizalisha katika ofisi za NEMC bila kuchukuliwa hatua."

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel Gwamaka amewataka wananchi kufuata Kanuni na Sheria za Uhifadhi wa Mazingira kwa kudhibiti viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali hususani kumbi za starehe na makanisa pamoja na kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku kwani ni chanzo cha uchafuzi wa mazingira.

Amesisitiza kuwa "wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mifuko ya plastiki wahakikishe kuwa viwanda vyao vinasajiliwa na Baraza na kupata cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira kabla ya kuanza uzalishaji na kufuata matakwa ya Sheria na viwango sahihi vilivyowekwa."

Pia ametoa angalizo kwa wazalishaji na wasambazaji wa mifuko ya plastiki kunisalimisha kwani Baraza litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa juu ya uwepo wa kiwanda au wasambazaji wa mifuko na vifungashio visivyokidhi viwango.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Athuman Ngenya amesema "wale wote wanaomiliki viwanda vya kuzalisha plastiki ambao wana leseni ya TBS endapo watahitaji kuhuisha leseni au kuchukua leseni mpya lazima wawe na Cheti cha Mazingira kutoka NEMC.

Nao wadau wa mazingira walitoa maoni yao juu ya udhibiti wa viwango vya kelele na mitetemo kwa kuomba kupatiwa vifaa vya kupimia sauti, kuboreshaji njia za utoaji elimu kwa wananchi ili kuwezesha kudhibiti kelele chafuzi pamoja na kupewa vibali maalum ili kuwezesha viongozi katika ngazi za mtaa kuchukua hatua stahiki kwa wanaokiuka Sheria.

Kwa upande wa katazo la mifuko ya plastiki wadau wameisihi Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahihi juu ya mifuko iliyopigwa marufuku na pia kuboresha njia bora za kuwadhibiti wale wote wanaozalisha mifuko ya plastiki kwa kuwachukulia hatua za Kisheria ili kuweza kutokomeza tatizo hili.
Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment