Atakayekwamisha Wafanyabiashara ni adui namba moja wa Serikali

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Afisa yeyote wa Serikali atakayekwamisha ufanyaji biashara, uwekezaji au uanzishwaji viwanda nchini ni adui namba moja wa Serikali na atachukuliwa hatua za kisheria.

Vilevile, Ametoa wito kwa watendaji hao kuwezesha uwekezaji, ufanyaji biashara, uanzishaji viwanda na kuhakikisha kila mwekezaji anapata anachostahili kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.

Dkt. Abdallah ameyasema hayo Septemba 25, 2023, wakati akiongoza Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi inayojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Fedha, Mipango na Uwekezaji, Kilimo na Katibu Tawala Mkoa wa Kagera walipotembelea Kiwanda hicho kuona hali ya uwekezaji na kutatua changamoto walizonazo.

Aidha, Dkt. Abdallah amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameweka Sera na Mazingira wezeshi katika ufanyaji biashara uwekezaji na uanzishaji wa viwanda ili kuiwezesha Tanzania kujitosheleza katika mahitaji ya bidhaa muhimu na kuuza ziada nje ya nchi na kutimiza malengo ya Tanzania kuilisha Dunia.

Akifafanua zaidi, Amesema Serikali imeanza kutimiza malengo hayo kwa kuanza na Sekta ya Sukari ambapo Kiwanda cha Sukari cha Kagera kinauwezo wa kizalisha tani 150,000 kwa mwaka katika 2023/2024 na kinapanga kizalisha tani 300,000 kwa mwaka kitakapokamilisha upanuzi wa awamu ya nne na hivyo kuchangia kuifanya Tanzania kutokuagiza sukari nje ya nchi, kuongeza ajira na pato la taifa hususan fedha za kigeni.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Bw. Tobi Nguvilo amesema uongozi wa Mkoa huo uko tayali kumlinda, kumtunza, kumsaisia na kuhakikisha hakwami kwa jambo lolote Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera kwa kuwa Mkoa huo unakitegemea kiwanda hicho kwa ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii kwa kuajiri wananchi 115,000 kutoka Mkoani humo pamoja na utoaji wa huduma bora za shule na hospitali.

Vilevile, Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari na Mmiliki wa Kiwanda cha Sukari Kagera Bw.Self Ally Seif amesema anaungana mkono juhudi za Serikali kwa katika kuwawezesha wawekezaji ili kitimiza dhamira ya kuiwezesha Tanzania kuilisha Dunia kwa kuanza na Sekta ya Sukari inayotoa ajira nyingi na kuongeza pato la taifa zikiwemo fedha za kigeni.

Mkuu wa Shule ya Malezi Bora ya inayomilikiwa Kiwanda cha Sukari Kagera akieleza maendeleo ya Shule hiyo kwa Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah inayojumuisha Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Tobi Nguvilo wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof. Kenneth Bengesi pamoja Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari na Mmiliki wa Kiwanda cha Sukari Kagera Bw.Self Ally Seif walipotembelea shule hiyo wakati wa ziara ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Septemba 25, 2023 Mkoani Kagera kwa lengo la kujifunza na kuona hali ya uwekezaji katika Kiwanda hicho.

Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Tobi Nguvilo wakiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwasa kuhusu maendeleo ya Mkoa huo Septemba 26, 2023 baada ya ziara ya kutembelea Kiwanda cha Sukari cha Kagera mkoani humo.

Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Tobi Nguvilo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof. Kenneth Bengesi pamoja Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari na Mmiliki wa Kiwanda cha Sukari Kagera Bw.Self Ally Seif.

Kamati hiyo na ujumbe wake ilitembelea mashamba ya miwa yanaoendeshwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera wakati wa ziara yao iliyofanyika Septemba 25, 2023 Mkoani Kagera kwa lengo la kujifunza na kuona shughuli za uandaaji, upandaji na umwagiliaji katika mashamba hayo ya miwa na upanuzi wa mashamba hayo yenye hekta 32,000 kati ya hizo 23,000 zinatumika.

Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Tobi Nguvilo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Prof. Kenneth Bengesi pamoja Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari na Mmiliki wa Kiwanda cha Sukari Kagera Bw.Self Ally Seif wakitembelea sehemu za uzalishaji sukari wakati wa ziara yao katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Septemba 25, 2023 Mkoani Kagera kwa lengo la kujifunza na kuona hali ya uwekezaji katika Kiwanda hicho.

Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw Tobi Nguvilo wakiwa pamoja na Menejimenti ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera wakipokea Taarifa ya maendeleo ya uzalishaji na upanuzi wa kiwanda hicho pamoja na kusikiliza changamoto na kuzitatua wakati walipotembelea Kiwanda hicho Septemba 25, 2023 Mkoani Kagera


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiongoza Kamati Maalum ya Katibu Mkuu Kiongozi inayojumuisha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Mipango na Uwekezaji, Kilimo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji Sukari na Mmiliki wa Kiwanda cha Sukari Kagera akiwa na wafanyakazi wa Hospitali ya Kiwanda hicho walipoitemblea Hospitali hiyo wakati wa ziara ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Septemba 25, 2023 Mkoani Kagera kwa lengo la kujifunza na kuona hali ya uwekezaji katika Kiwanda hicho.

Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment