KATIBU MKUU MSIGWA ATEMBELEA TaSUBa

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa amefanya ziara na kutembelea Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo amefurahishwa na uendeshwaji wa Chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani, Mhe.Msigwa amesema taasisi hiyo inatakiwa kuendelea kufanya ubunifu ili iwashawishi na kuwavutia wasanii kuja kuongeza maarifa.

Aidha amesema kuna baadhi ya wasanii wanafanya vizuri lakini hawana elimu ya sanaa hivyo wanatakiwa kupewa ushawishi na kuweza kujiunga TaSUBa.

Serikali ipo tayari kuanzisha vituo vya utamaduni na sanaa katika mikoa yote ya Tanzania. lengo ni kuhakikisha wizara inaendelea kulinda utamaduni na kuwapa fursa wasanii kujifunza zaidi". Amesema

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TaSUBa, Bw.George Yambesi amesema wataendelea kufanya utafiti kuhusu sanaa ikiwemo kuhifadhi kazi za wasanii mbalimbali na pia wanatarajia kuendelea kushirikiana vyema na wizara kuhakikisha wanakabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

"Wasanii wanatakiwa kuigeuza sanaa kuwa kazi ikiwemo kujiendeleza kitaaluma hapa TaSUBa na vilevile tutaendelea kufanya utafiti kuhusu sanaa ikiwemo kuhifadhi kazi wasanii mbalimbali zitakazosaidia vizazi vya baadaye". Amesema
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akipiga ngoma na baadhi ya wasanii wakati alipotembelea Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akijaribu kuitumia video camera katika studio wakati alipotembelea Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Dkt Herbert Makoye wakati alipotembelea chuoni h leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akizungumza na wasanii wa ngoma za asili wakati alipotembelea Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akiwa katika studio za Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakati alipotembelea Chuoni hapo leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya ushauri Chuo Cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) wakati alipotembelea chuoni hapo leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TaSUBa, Bw.George Yambesi akizungumza mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Gerson Msigwa kutembelea TaSUBa leo Oktoba 12,2023 Bagamoyo mkoani Pwani.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment