MAMALISHE 1000 WASHIRIKI MASHINDANO YA KUPIKA KWA GESI YA ORYX MKOANI MBEYA

MAMALISHE 1000 mkoani Mbeya ambao wanashiriki mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx huku Kampuni ya Oryx Gas ikisisitiza lengo la mashindano hayo ni kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi kama ambavyo Rais Dk.Samia amedhamiria ifikapo mwaka 2024 asilimia 80 iwe inatumia nishati hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa leo Agosti 27,2024 jijini Mbeya , Meneja Miradi ya Nishati Safi kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Peter Ndomba amesema mashindano hayo yanatija kubwa kwa Mama Lishe na Baba Lishe kwani wanatambua kundi hilo ndilo linaloathirika kiafya kutokana na kutumia kuni na mkaa kwa muda mwingi.

"Mama Lishe anakaa muda mrefu katika anapopika kwa kutumia na mkaa kwani tunaambiwa wananchi wengi wa Tanzania wanafariki kila mwaka kwa kutokana na matatizo ya kupumua au matatizo ambayo yanatokana na madhara ya kuni na mkaa.

"Sasa katika hao watu tunaweza kusema Mama Lishe ndio waathirika wakubwa , kwa hiyo ni jamii ambayo sasa hivi sisi Oryx tunamkakati wa kuhamasisha iachane na kuni na mkaa kwasababu wao wanakaa muda mrefu katika kupika kila siku ndani ya siku 365,"amesema Ndomba.

Amesisitiza kwa hiyo Mama Lishe na Baba Lishe wakiamua kubadilika na kuanza kupila kwa nishati safi kutawasaidia kukabiliana na changamoto za kiafya na hivyo kuokoa maisha yao, hivyo mashindano ya kupika kwa gesi ya Oryx kunalenga kuliepusha kundi hilo dhidi ya madhara yanayotokana na kuni na mkaa.

"Lengo la mashindano haya ni katika muendelezo uleule ambao Oryx tumeuanza muda mrefu wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika mapishi yake.

Kwa hiyo ujumbe wetu kwa watu watumie gesi katika kupika mapishi.Tunaamini nishati safi ya kupikia ni suluhisho la changamoto nyingi hasa za kiafya,kimazingira na kiuchumi,"amefafanua.

Pia amesema Oryx wanaamini wanalojukumu la kuendelea kuhamasisha nishati safi na ndio maana tumeleta mashindano haya katika eneo la wazi ili kila mtu aone .

Kwa upande wao baadhi ya Mama na Baba Lishe wanaoshiriki mashindano hayo wamempongeza Mbunge wao Dk Tulia Akson pamoja na Oryx Gas kwa KUANDAA mashindano hayo ambayo yanakwenda kuongeza hamasa ya matumizi ya nishati safi katika shughuli zao za kupika.

Akizungumza kuhusu mashindano hayo Mama Lishe Yusra Ismail anayefanya shughuli zake za mama Lishe eneo la Sabasaba jijini Mbeya amesema mashindano hayo yanamanufaa makubwa kwao kwani wanapata elimu kuhusu umuhimu wa kutumia nishati safi lakini na matumizi salama ya nishati hiyo.

"Gesi ya Oryx imekuwa ikitusaidia katika shughuli zetu za mapishi, tunafanya shughuli zetu kwa haraka,"amesema huku akieleza kutumia kuni na mkaa kunapoteza muda lakini pia wanaathirika kiafya.

Ameongeza kuwa wanamuunga mkono Rais DK.Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi nchini kwasababu nishati ya gesi ni nzuri na inasaidia katika shughuli zao.

Wakati huo huo Mama Lishe Sabrina Anold anayetokea Kata Ilomba ameseema programu ya nishati safi ya kupikia katika Jiji la Mbeya imekuwa na faida nyingi kwani Mama na Baba Lishe wameendelea kuhamasika kwa kutumia nishati safi ya kupikia katika shughuli zao.

"Dk.Tulia kwa kushirikiana na Oryx Gas wametusaidia sana kwani awali tulikuwa tunatumia kuni na mkaa ambapo tulikuwa tunapoteza muda ,kwahiyo baada ya kuja nishati safi tunaweza kutumia muda mzuri na kingine imetusaidia katika eneo la afya kwani wengine macho yamepoteza kuona vizuri kwasababu ya Moshi kwa kutumia kuni." .

Wakati huo huo Baba Lishe Yusuph Maumba ambaye ni mshiriki wa shindano la mapishi amesema mashindano hayo yanaongeza hamasa ya kutumia nishati safi ya kupikia na hasa gesi ili kuepuka kuharibu mazingira kwasababu ya kupika kwa kuni na mkaa.

"Kiukweli tutandelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia kwa kutunza mazingira kwa kutumia nishati ya gesi katika kupikia na uzuri chakula kinachopikwa kwa gesi ni kizuri na kitamu . Nimefurahishwa sana na mashindano hayo."

Ameongeza kuwa kutumia kuni na mkaa kunachangamo nyingi kwanza mkaa ni wa msimu kwasababu nyakati za mvua mkaa unakuwa umeloa na wakati mwingine unauziwa chenga.

Kwa upande wake Baba Lishe Zakaria Msigwa amesema wanamuunga mkono Rais Samia kwa kutumia nishati safi ya kupikia sambamba na kuhamasisha wengine kutumia nishati hiyo kwani dhamira ya Rais ni kuona wananchi wake wanatumia nishati safi ya kupikia na kuachana na nishati chafu.

Amewashauri wanaotumia kuni na mkaa kuachana na matumizi ya nishati chafu na kisha kuanza kutumia nishati safi huku akiwaomba Oryx kuendelea kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia nishati pamoja na kuendelea kugawa mitungi ya gesi na majiko yake.
Share on Google Plus

About emmanuel mbatilo

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment