NEC KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA WAGOMBEA WANAOFANYA KAMPENI KWA LUGHA ZA MATUSI

Na Asha Said, DAR ES SALAAM                        
MKURUGENZI wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Wilson Mehera Charles amesema kuwa kuna baadhi ya wagombea wamekuwa wakifanya kampeni  zao kwa kutoa lugha za matusi, vitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na vyama hivyo kufungiwa kufanya kampeni.
Mahera alisema hayo  jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano  wa siku moja kwa vyombo vya habari za mitandaoni. 
Alisema, katika kipindi hiki cha kampeni kuna  baadhi ya vyama vimekuwa vikitoa lugha za matusi na za uzalilishaji jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uchaguzi. 
Alisema japo hiki ni kipindi cha kampeni, lakini sheria nyingine zote zinaendelea kufanya kazi hivyo hawatasita kuchukua hatua. 
Mahera alisema kabla ya uchaguzi vyama vyote vilisaini maadili ya uchaguzi, hivyo atakayefungua atakuwa anajua maana  chama chake kilisaini fomu hiyo maalum ya uchaguzi.                           
"Sisi kama NEC tukiona kama kuna chama kinatoa  matusi kwenye kampeni badala ya kunadi sera tutakifungia chama hicho kufanya kampeni, kwa kuwa kila hata mgombea anajua kuhusu fomu aliyosaini kwa ajili ya maadili ya uchaguzi,"alisema.  
Aidha, amewapongeza watoa huduma mitandaoni kwa kutoa taarifa za uchaguzi na kwamba  watoa huduma mitandaoni ni wadau muhimu wa uchaguzi na kuwataka kuhakikisha utoaji taarifa unakuwa uendelevu kudumisha amani. 
Amevitaka vyombo hivyo kuendelea kuhamasisha watanzania ili wajitokeze siku ya uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura na kwamba ushirikiano na vyombo hivyo utafanikisha mchakato mzima wa uchaguzi. 
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment