MUGABE ASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 90 KWA KUMKUMBUKA HAYATI MWALIMU J.K NYERERE

 Maelfu wa wananchi wa Zimbabwe walijitokeza kwenye uwanja wa Marondera kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Rais wa nchi hiyo wakati akitimiza miaka 90, ambapo sherehe hiyo imegharimu kiasi cha dola milioni 1 za Kimarekani. Kiongozi huyo mwenye miaka 90, alikuwa akiongea kwenye sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika jana nchini Zimbabwe muda mfupi baada ya kuwasili kutoka Singapore alikokuwa amelazwa akifanyiwa upasuaji wa macho. 
***********************************
Alipokuwa akizungumza katika sherehe hiyo, Kiongozi huyo aliyetimiza miaka 90 na mwenye miaka 34, ndani ya uongozi kama Rais wa Zimbambwe,  alisema viongozi wa Afrika wanapaswa kufanya zaidi kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere aliyeifanya Tanzania kimbilio la vuguvugu la ukombozi barani Afrika. 
“Nataka kusema, wakati ambapo heshima zimekuwa zikimwagwa kwa mashujaa wa Afrika, mtu anayeonewa ni Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Mugabe.
 “Hapa tulipo, vuguvugu za ukombozi, kule tulikotoka tulitegemea msaada wa Tanzania. Lakini hakuna kinachosemwa kuhusu mtu huyu na nchi yake kwenye Jumuiya ya Afrika.”
Mugabe ambaye ni makamu mwenyekiti wa AU, alisema bara la Afrika linapaswa kukumbushwa fadhila inazotakiwa kumlipa Mwalimu Nyerere.
“Nataka sisi Wazimbabwe, kusimama kwaajili ya Nyerere.  Afrika inatakiwa kukumbushwa wajibu iliomtupia mtu huyu, mzigo wa kuendesha vuguvugu zote za ukombozi,” alisema. “Mwisho wa siku, hakuna hata mmoja anayesema Tanzania ilistahili japo kutajwa tu kwa kufanikisha mission hii, mission ya kuwa nasi kama marafiki, mission ya kutufanya tuendeshe vuguvugu za ukombozi wa Afrika. 
Wote tulienda kwa njia tofauti, kwa sura tofauti hadi Tanzania kukomboa nchi zetu na hatujaenda tena Tanzania. Well, naenda kuwa mwenyekiti wa AU, ntashughulikia suala hili,” alisema.
“Hakuna aliyetambua kile Nyerere alichokifanya. Sisi wa Wazimbabwe sio wachoyo wa shukrani, ni taifa lenye shukrani na tutamuenzi mtu huyu.”
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment