RAIS KIKWETE ATOA URAIA KWA WAKIMBIZI 162,000 WA BURUNDI - ATUA DODOMA KUONGOZA VIKAO VYA CCM

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wakimbizi 162,000 kutoka Burundi waliopatiwa hati za uraia wa Tanzania katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Tabora jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati ya Uraia wa Tanzania Bi.Bizimana Nyakiki Naluka, ambaye ni  mmoja kati ya wakimbizi 162, 000 kutoka Burundi waliopatiwa uraia wa Tanzania katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Tabora jana.
 Baadhi ya Wakimbizi 162000  kutoka Burundi walipatiwa uraia wa Tanzania jana mjini Tabora.
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya CCM. Wapili kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na watatu kushoto ni Makamu wa CCm Bara Ndugu Philip Mangula.
 Vijana wa CCM wa mkoa wa Dodoma wakimvika skafu na kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo anatarajiwa kuongoza vikao vya ngazi ya juu vya CCM.
Rais Kikwete akikaribishwa na vijana wa ccm mkoa wa Dodoma, wakati akiwasili 
mjini Dodoma akitokea mkoani Tabora leo mchana.
 Picha na Fredy Maro

Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment