OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA ZA MFUMUKO WA BEI NCHINI

 Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
Baadi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia suala la mfumuko wa bei nchini.
Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO
******************************************

Wananchi wameombwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kupitia ofisi za takwimu za mikoa wakati wa ukusanyaji wa takwimu mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa zilizo sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Kwesigabo amesema kuwa pamoja na mambo mengine Ofisi ya Taifa ya Takwimu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa taarifa za mfumuko wa bei nchini ambapo kwa mwaka huu unaonesha umepungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kuanzia kipindi cha mwezi Oktoba 2013 hadi Oktoba 2014. 

Kwesigabo amesema kuwa mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua bei kwa mwezi Oktoba 2014 zikilinganishwa na mwezi Oktoba 2013 ni pamoja na bei za mahindi asilimia 7.2, unga wa mahindi asilimia 5.5 na unga wa ngano asilimia 4.4.
Bidhaa nyingine za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni ulezi asilimia 3.5, tambi asilimia 2.2, samaki asilimia 4.6, mihogo asilimia 2.1 na sukari imepungua kwa asilimia 4.6.
Aidha, Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Oktoba 2014 umepungua hadi asilimia 5.9 kutoka asilimia 6.6 tofauti na hali ilivyokuwa mwezi Septemba 2014.
 “Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Oktoba 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka ulioishia mwezi Septemba 2014” alisema Kwesigabo.
Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na kupungua kwa asilimia 0.4 kama ilivyokuwa kwa mwezi Septemba mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zimepungua hadi kufikia 149.70 kwa mwezi Oktoba 2014 kutoka 149.93 za mwezi Septemba 2014.  
Kwesigabo amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na vitafunwa vinavyotokana na unga wa nagano kwa asilimia 2.4, unga wa mahindi kwa asilimia 0.1, samaki kwa asilimia 1.7,ndizi za kupika kwa asilimia 7.5, mbogamboga kwa asilimia 2.2, viazi mviringo kwa asilimia 1.5 na sukari kwa asilimia 1.6.
Aidha, amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii umefikia shilingi 66 na senti 80 kwa mwezo Oktoba 2014 kutoka mwezi Septemba 2010
Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua hadi kufikia asilimia 6.43 kwa mwezi Oktoba 2014 ikilinganishwa na asilimia 6.60 za mwezi Septemba mwaka huu, huku Uganda ikiwa na mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 1.8 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikilinganishwa na 1.4 za mwezi Septemba.
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment