JAJI WEREMA ANG'ATUKA


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, jana alitangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake hiyo ambapo ni kuanzia jana Jumanne, Desemba 16, 2014.
Kwa maamuzi ya Jaji Werema, tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu na kumpa baraka zote.
Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema, alisema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na kusababisha kutokea kwa mtafaruku huo uliokuwa ukiendelea Bungeni na kuchafua hali ya hewa.


Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake akiwa kazini na kuongoza na uaminifu na uadilifu.
Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment