MAGUFULI ACHUKUA FOMU YA URAIS, RAIS JK ASEMA; "USHINDI UPO"

Na Pendo Omary, DAR ES SALAAM
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.John Pombe Magufuli ambaye aliambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu leo amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). 
Msafara wa Magufuli na Suluhu ulifika katika ofisi za NEC saa 5.43 asubuhi huku ukisindikizwa na makada wa chama hicho wakiwemo: Katibu Mkuu, Abrahaman Kinana, Katibu Mwenezi, Nape Nnauye, Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro; Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq.
Magufuli akiwa mgombea mwenza wake, Samia 

PICHA ZAIDI GONGA HAPA



Aidha, ulinzi uliimalishwa huku askari polisi waliokuwa na silaha za moto wakizunguka jirani na ofisi za NEC.
Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, wagombea hao walitumia muda wa dakika 27 kukamilisha zoezi la kuchukua fomu kisha kurejea katika viwanja vya ofisi za CCM makao makuu Lumumba kuungana na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliyeongozana na mkewe Salma Kikwete, kuhutubia mamia ya wanachama wa chama hicho waliojitokeza kuwasindikiza wagombea kuchukua fomu.
Akizungumza baada ya kukaribishwa na Kinana, Rais Kikwete alinzakuzungumza huku akivirushia dongo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwamba wamechukua “makapi ya CCM” huku akisema, “ Wale wanaodhani CCM ni ya mchezo watakiona cha mtema kuni.
Huku akiongeza kuwa watu wenye tama kupitiliza Tumejiandaa vya kutosha na tutashinda. Uwezo tunao, maarifa tunayo tutashinda. Tujipange kwa hoja za kuzungumzia uzuri wa CCM.”
“CCM jiandaeni kushangilia ushindi….Utawala bora upo, demokrasia ipo, uhuru wa habari upo, watu wanajiunga na vyama vya siasa kwa uhuru, uchumi unakuwa na maendeleo yanaendelea kupatikana,” amesema Rais Kikwete.
Kwa upande wake Magufuli amesema, “leo tumechukua fomu, tutaizungusha kuweza kupata wadhamini. Nimepokea kijiti hiki kwa mikono miwili. Mategemeo ya watanzania ninayajua. Uongozi wa awamu ya nne uliweka msingi mzuri. Nitaipeperusha vizuri CCM kwa maslahi ya watanzania wote bila kujali chama,” amesema Magufuli.

Share on Google Plus

About Mahmoud Bin Zubeiry

Mahmoud Zubeiry Works at BIN ZUBEIRY "BIN ZUBEIRY" Tangaza nasi hapa.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment